Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, May 17, 2010

LEO NI SIKU YA MAWASILIANO NA JAMII HABARI DUNIANI



Katibu Mkuu wa ITU Dr. Hamadoun I. Toure (wa pili kulia) akipokea zawadi maalamu kutoka kwa Naibu Waziri wa ICT wa China wakati wa Chakula Maalum cha kuadhimisha mkesha wa maadhimisho ya siku ya TEKNOHAMA duniani katika Hoteli ya Taifa ya Shanghai (State Hotel Shanghai iliyoko katika kitongoji cha Pudong



Katibu Mkuu wa ITU Dr. Hamadoun I. Toure (wa pili kutoka kulia) akiwa na wawakilishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania wanaohudhuria Maadhimisho ya siku ya TEKNOHAMA katika Hoteli ya Serekali ya Shanghai. Kulia ni Dr. Justinian Anatory, Mjumbe wa bodi ya TCRA, kushoto ni Dr. Joseph Kilongola, Mkurugenzi wa ICT wa TCRA na wa pili kushoto ni Bwana Innocent Mungy, Meneja Mawasiliano wa TCRA.


Na Ripota wa Globu ya Jamii, Shangai
Leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya Mawasiliano Jamii Habari Duniani, nchi zote duniani zinaadhimisha siku hii muhimu kwa maendeleo ya dunia yetu kwa shughuli mbalimbali, ikiwemo maonesho na makongamano yaliyojikita katika kujadili kauli mbiu ya maadhimisho ya Mwaka huu, "Miji Bora, Maisha Bora na TEKNOHAMA".
Maadhimisho haya yanafanyika kimataifa katika jiji la Shanghai ambako kuna maonesho makubwa ya kuadhimisha kauli mbiu ya mwaka huu kwa vitendo katika kila sekta, yenye lengo la kuonesha umuhimu wa kuwa na miji na makazi bora katika kuboresha maisha ya watu duniani.
Kauli mbiu ya mwaka huu, hususani kwa sekta ya Mawasiliano, inakusudia kutoa changamoto katika kuhakikisha serikali mbalimbali duniani zinajipanga kuwaletea wananchi wake maendeleo kwa kupanga na kujenga miji bora ili kuboresha maisha.Tanzania haiwezi kubaki kama kisiwa, ni muhimu tuimarishe matumizi ya TEKNOHAMA katika shughuli zetu zote za maendeleo hsusani katika kupanga miji yetu na matumizi mazuri ya TEKNOHAMA kwa maendeleo ya Taifa letu.
Jana jioni katika dhifa ya kitaifa ya kukaribisha siku ya maadhimisho haya, Katibu Mkuu wa ITU (International Telecommunications Union) Dr. Hamadou Toure alitaka dunia kuangalia kwa makini umuhimu wa kutumia TEKNOHAMA katika kuboresha miji duniani ili kuwa na maisha bora. Taarifa Maalumu ya Katibu Mkuu huyo inafuatia hapa chini.

No comments:

Post a Comment