Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, May 10, 2010

wimbo wa shakira wadoda south africa


Mwanamuziki wa Pop Shakira a.k.a Kiuno bila mfupa.

Wimbo maalum wa Kombe la Dunia ulioimbwa na mkali wa Pop,Shakira unaojulikana kwa jina la “Waka Waka” umepata mapokezi mabaya kutokana na kutokubalika nchini Afrika ya Kusini.

Katika wimbo huo ambao Shakira ameishirikisha bendi ya Freshlyground ya Sauzi ulizinduliwa wiki iliyopita katika vituo vya redio lakini haujaonyesha kukubalika “Ni mbaya,sikubaliani nao kwa nini wampe yeye aiwakilishe Afrika,mbona wapo Waafrika wengi wenye uwezo,”alisema mkazi wa Soweto aliyejitambulisha kwa jina la Lindi Munonde.

Shakira,33 ameimba wimbo huo na pia anatarajia kutumbuiza katika onyesho maalum litakalofanyika Juni 10 kwa ajili ya uzinduzi wa fainali hizo.Wakazi wengi wan chi hiyo wamekuwa wakipinga kitendo cha wasanii wazawa kutopewa kipaumbele katika kutumbuiza,jambo ambalo Kamati ya Mashindano limeahidi kulifanyia kazi

Habari hii ni kwa msaada wa Mtandao.

No comments:

Post a Comment