Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, May 23, 2010

Meya jiji la Mwanza mbaroni kwa mauaji!!


Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Leonard Bihondo, leo amesomewa shitaka la mauaji ya Katibu wa CCM ngazi ya Kata, katika mahakama ya mwanzo ya Kata ya Isamilo mkoani Mwanza, sambamba na watuhumiwa wengine watatu.
Akifafanua kiini cha mkasa huo, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza SAPC Simon Sirro amesema mtuhumiwa Leonard Bihondo na wenzake Jumanne Oscar, Baltazari Shushi na Abdulah Hausi walimuua Bahati Stephan katibu wa CCM Kata ya Isamilo Mei 14 mwaka huu, kwa kumchoma kisu akiwa ofisini kwake.

Katika shauri hilo linalosimamiwa na wakili wa Serikali Stephen Kakwega, watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote, kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kuendesha kesi hiyo na wamerudishwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena.

Hili ni mojawapo ya matukio makubwa matatu nchini kwa viongozi wakubwa wa Serikali kujihusisha na mauaji ya raia, ambapo licha ya kesi iliyokuwa ikimhusu kamanda Abdalah Zombe aliyeshutumiwa kuwaua Wafanyabiashara kwa kisingizio cha ujambazi,

kadhalika miaka ya hivi karibuni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kigoma marehemu Kapteni Ditopile Ukiwaona Mzuzuri alifikishwa mahakamani kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua dereva wa daladala katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

Kapteni Mzuzuri alifariki baadaye tarehe 20 April 2008 kwa kuugua ghafla akiwa hotelini na mkwewe mjini Morogoro, wakati kesi ilipokuwa ikiendelea.

No comments:

Post a Comment