Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, May 25, 2010

Sasa binadamu wa kutengenezwa waja!


Mabingwa wa mambo afya chini ya ardhi ya Uncle Obama (Marekani) kwa mara ya kwanza tangu zama za Adam na Hawa wamefanikiwa kuunda seli hai (living cell) kwa kutumia vinasaba vilivyotengenezwa na binadamu(manmade DNA) iliyounganishwa na vitu mbalimbali.

Hali hiyo ambayo inatafsiriwa na wengi kuwa ni mwanzo wa utengenezaji wa uhai bandia..imeshazua mijadala chungu tele duniani hasa baada ya tamko la mabingwa hao.

Habari zaidi zinasema kuwa katika ugunduzi huo wataalamu hao waliunda programu ya vinasaba na kuvipandikiza ndani ya seli pokezi.

Ilielezwa kuwa baada ya hatua hiyo matokeo yake yakazaa vijiumbe maradhi vinavyofuata nyenzo ileile ya DNA iliyounganishwa.

Ugunduzi huo uliochapishwa katika jarida maarufu liitwalo 'science', umeshangiliwa na ulimwengu wa sayansi kama hatua kubwa, ingawa wakosoaji wanasema viumbe sanisia vinaweza kusababisha madhara yasiyoelezeka huku wengine wakisema kuwa manufaa ya teknolojia hii yametiwa chumvi.

Hata hivyo wataalamu hao wanasema kuwa wana nia ya kuunda seli za bakteria hiyo ambayo itasaidia katika utengenezaji wa dawa, mafuta na kumeza gesi zinazochafua mazingira.

No comments:

Post a Comment