Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, May 19, 2010

Inspekta Said Mwema na Balozi wa Uingereza wazindua Programu Ya Mafunzo Ya Uongozi Kwa Jeshi La PolisiBalozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner, pamoja na Inspecta Generali wa Polisi, (IGP) Saidi Mwema wamezindua programu ya mafunzo ya uongozi kwa Jeshi la Polisi la Tanzania inayodhaminiwa na Serikali ya Uingereza.

Mafunzo hayo, ambayo yataendeshwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Kuboresha Idara ya Polisi ya Uingereza (NPIA) pamoja na ile ya Hampshire kwa muda wa miezi tisa (kuanzia mwezi ujao), yatakuwa na lengo la kubadilishana uzoefu na mbinu bora - kwa kujikita zaidi katika masuala ya kiuongozi na kimenejimenti.

“Mafunzo hayo ni muhimu sana kwetu hasa kwa kipindi hiki cha maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao, lakini pia ni muhimu zaidi katika jukumu zima la kudumisha amani hapa nchini,” alishukuru IGP Saidi Mwema.

No comments:

Post a Comment