Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, May 25, 2010

Magari ya JK ni mikweche au ya kichinaaaa???


Ziara ya mkuu wa nchi aliyoifanya jana mkoani Dsm iliingia kizungumkuti baada ya gari alilotumia kwenye msafara wake kuzimika ghafla mara mbili barabarani.

Gari hilo lilizimika kwa mara ya kwanza katika makutano ya barabara ya Morogoro na Mavurunza wilayani Kinondoni eneo la Kimara Mwisho majira ya saa 7:30 mchana ambako msafara wake ulisimama kwa dakika tatu.

Gari hilo lilizimika tena kama hatua 150 tu kutoka katika makutano hayo na ndipo rais akahamishiwa kwenye gari lingine lililokuwa kwenye msafara huo huku akiwa ananyeshewa mvua.

Tena majira ya saa 10:00 jioni msafara wake uliokuwa ukitokea Keko Toroli wilayani Temeke, ulikwama tena maeneo ya BP barabara ya Kilwa ambako gari hilo jipya nalo lilizimika ghafla.

Tukio hilo la kihistoria nchini, liliwapa wakati mgumu maafisa usalama ambao kila mara gari lilipokuwa limezimika, walishuka kwenye magari yao na kuondoa bendera na ngao.

Kusimama gafla kwa msafara wake eneo la Kimara, kulimlazimisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya kukimbilia eneo alilokuwapo rais huku umati wa watu uliokuwa umejibanza pembeni mwa barabara nao ukisogea karibu.

Ilimchukua takriban dakika mbili kwa maafisa wa usalama wa taifa kupata suluhu ya namna msafara huo utakavyoendelea kutokana na mkanganyiko wa gari ipi kati ya mbili zilizokuwa zinafanana aiangie rais.

Msafara huo uliendelea baada ya Rais Kikwete ambaye alikuwa amevaa shati la kitenge la mikono mirefu na akiwa analowa hasa miguuni kuhamishiwa katika gari jingine huku lile lililoharibika likiwa linasukumwa na umati wa watu hadi pembezoni mwa barabara.

Hata hivyo, baada ya dakika nane gari hilo aina ya Toyota Landcruiser VX V8 lililokuwa na rangi nyeusi, liliwaka baada ya dereva kujaribu kuliwasha kwa zaidi ya mara nne.

Kuzimika kwa gari lake eneo la PB kulifanya msafara wa rais usimame kwa takriban dakika kumi kabla ya kuendelea.

2 comments:

  1. Hi there just wanted to give you a quick heads up. The words in your post seem to be running off the screen in Opera.
    I'm not sure if this is a format issue or something to do with internet browser compatibility but I figured I'd post
    to let you know. The layout look great though!
    Hope you get the problem resolved soon. Many thanks

    Feel free to visit my homepage - laser cellulite treatment

    ReplyDelete
  2. rosacea laser treatment South Amboy

    my web blog: rosacea laser treatment Wounded Knee

    ReplyDelete